Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:30 pm

UTAFITI: MADHARA YA KUTOPATA USINGIZI MUDA MREFU.


1. Maumivu ya kichwa
2. Kuongezeka uzito, kutokana na kuongezeka kwa hamu ya kula na kutamani vyakula vyenye mafuta mengi.
3. Matatizo ya macho, macho kuuma na pia kuwa mekundu kutokana na kukatisha usingizi na pia huvimba.
4. Magonjwa ya moyo. Unapokosa muda wa kulala wa kutosha msukumo wa damu (BP) huongezeka na hatimaye hupelekea matatizo ya moyo.
5. Uwezo wa kufikiri hupungua, hii ni kutokana na kutokuupatia ubongo muda wa kupumzika na kutafakari.
6. Ajari, unapoendesha gari unakuwa katika hati hati ya kupata ajari kwani utaendesha ukiwa una uchovu na usingizi kutokana na kila siku unakatisha usingizi.
7. Kisukari, kutokupata muda wa kutosha wa kulala husababisha baadhi ya “organ” za mwili kutokufanya kazi ipasavyo na hivyo kupelekea mwili kupata kisukari.
8. Matatizo ya kumbukumbu. Utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa watu wanao lala sana husahau kidogo. Hivyo basi ukosefu wa usingizi hupelekea mtu kupoteza kumbukumbu.
9. Kuzalisha mkojo kwa wingi, mtu asiepata usingizi wa kutosha huzalisha sana mkojo na hii ndio sababu kubwa kwanini mtu wakati wa usiku hakojoi sana ukiringanisha na mchana. .
10. Kifo, kutokulala muda unaotakiwa ambao ni masaa 7 hadi 8 hupelekea kufa mapema zaidi ya yule amabaye analala kwa muda unaotakiwa.


Kukosa usingizi na kutokulala vizuri mara kwa mara husababisha matatizo mengi kiafya katika muonekano, kumbukumbu, ngozi, uzito, akili na usalama katika mazingira. Yafuatayo ni matatizo ambayo unaweza kuyapata endapo utakosa usingizi mzuri kwa muda mrefu au kulala vibaya.
  • Ajali, kukosa husingizi kwa muda mrefu usababisha uchovu ambao unaweza pelekea kuumi katika mazingira na kazini.
  • Kuharibu uwezo wa kufikiria, hupunguza akili ya mtu kufikiria, kujifunza, kukumbuka vitu kwa haraka na kufanya maambuzi sahihi ya vitu.
  • Hatari ya kupata magonjwa, kukosa usingizi mara kwa mara umuweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa ya akili, moyo, presha, kiharusi, kisukari nk.
  • Kukosa hamu ya mapenzi, hii ni kwa wote wake kwa waume kwani uharibu mfumo mzima wa mapenzi na hormoni katika mwili na kupunguza au kumaliza hamu ya kufanya mapenzi.
  • Msongo wa mawazo, kukosa usingizi kwa muda mrefu usababisha huzuni, kufadhaika, maumivu ya kichwa, wasi wasi kukosa raha na amani asa kwa wale wanaolala chini ya masaa 6 kwa siku.
  • Kuzeesha ngozi, kukosa usingizi kwa muda mrefu usababisha ngozi kuwa na mikunjo, kubadilika rangi na kuzeeka na macho kuvimba.
  • Kuongezeka uzito, kwa kuongeza njaa na hamu ya kula ukufanya kuwa na uzito kupita kiasi.