November 29, 2024, 3:48 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
UTAFITI: HISTORIA YA SIKUKUU YA MWAKA MPYA.
Mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwaka na mara nyingi ni sherehe na nafasi ya watu kutakiana heri na baraka za mwaka mpya.
Katika tamaduni mbalimbali nafasi hii ni sikukuu moja au zaidi pasipo na kazi za kawaida.
Tarehe ya mwaka mpya inategemea kalenda yake:
- katika sehemu kubwa ya dunia inayotumia kalenda ya Gregori ni 1 Januari
- Uajemi, Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Azerbaijan, Turkmenistan na Kashmir husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiajemi kwenye sikukuu ya Nouruz ambayo ni sikusare ya bubujiko inayotokea kati ya tarehe 20 - 21 Machi kwenye kalenda ya Gregori lakini kwao mwezi na mwaka mpya unaanza
- Wachina na Wavietnam husheherekea mwaka mpya wakati wa mwezi mwandamu wa pili baada ya solistasi ya majira baridi na hii inacheza kati ya 21 Januari na 21 Februari.
- Nchi ya Israeli na Wayahudi husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya kiyahudi kwa jina la rosh hashana ambayo ni siku inayotokea kati ya Septemba na nusu ya kwanza ya Oktoba.
- Waislamu na nchi ya Saudia huwa na mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiislamu. Kalenda hii inafuata mwezi tu kwa hiyo sikuu zake huzunguka katika mwaka wa jua.
- Sikukuu ya Diwali inasheherekewa na jumuiya kadhaa pia kama mwaka mpya.
Nje ya mahesabu haya kuna kalenda nyingine zisizoanzisha mwaka kwa sherehe. Mifano ni:
- mwaka wa shule
- mwaka wa biashara ambako hesabu mpya inaanzishwa
- mwaka wa kanisa ambayo katika sehemu kubwa ya Ukristo unaanza kwenye jumapili ya Adventi (majilio) ya kwanza.
Newest Posts