Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:46 am

SUMAYE: DKT BASHIRU AJIANDAE KUCHUKIWA NDANI YA CCM

Dar es Salaam: Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema matamshi aliyoyatoa Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM, Dk Ally Bashiru ya kuwa vitendo vya rushwa na kutowajibika vinasababisha watu kupuuzia uchaguzi na kuuona kama ni maigizo ipo sahihi, lakini amemtahadharisha kuwa ajiandae kuchukiwa na Chama chake.

Sumaye anesema kuwa Katika mikutano yake mbalimbali na wanahabari aliwahi kusema kura ambazo CCM imepata katika uchaguzi wa 2010, chama hiki hakikuwa na uhalali wa kuwa chama tawala tena. Matokeo yake nikaanza kuchukiwa na kutopendwa ndani ya chama.

“Hii ndiyo dalili kubwa ninayoiona kwa Dk Bashiru ndani ya chama chake. CCM hawapendi kuambiwa ukweli kwa sababu wanaona watashindwa katika utekelezaji wa majukumu yao mbalimabli,” alisema Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Hanang’.

Alisema alichokizungumza Dk Bashiru ni kujaribu kukitahadharisha chama chake ili kifanye kazi na kubadilisha misimamo yake kusudi kiendelee kuaminiwa na wananchi.

“Ni vema Dk Bashiru ameyasema haya. Lakini wangesema wapinzani tungeitwa wachochezi na kesho yake unaitwa na vyombo vya dola kuhojiwa,” alisema Sumaye.