- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: RAFIKI WA MESSI HATARINI KUUWAWA
Mtoto wa Kipakistan aliyepata umaarufu mkubwa mitandaoni baada ya kuwa shabiki wa kutupwa wa mchezaji nyota wa kandanda Duniani Lionel Messi amelazimika kutoroka nyumbani yeye na familia yake, hii ni baada ya familia yake kupokea vitisho kutoka kwa kundi lenye itikadi kali la Taliban.
Murtaza Ahmadi mwenye mika saba alipata umaarufu mwaka 2016 baada ya kupigwa picha akiwa amevalia mfuko wa plastiki unaofanana na jezi ya mchawi Messi.
Baadae alikutana na nyota huyo nchini Qatar.
Walikuwa wakiishi kusini mashariki mwa mkoa wa Ghazni - ambao umekuwa ukilengwa na wanamgambo wa Talin - sasa wamekimbilia mji mkuu wa Kabul.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP familia hiyo ilijaribu kutoroka mwaka 2016 lakini ikarejea tena mkoani humo baada ya kuishiwa na pesa za matumizi.
Murtaza alikuwa na miaka mitano wakati alipovalia tishet ya mfuko wa plastiki uliyo na ransi ya bendera ya ya timu ya taifa ya Argrntina ambayo nahodha wake ni Messi
Baada ya picha hiyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii watu walitoa wito wa kumuomba Messi kukutana nae,wito ambao nyota huyo aliuitikia.
Jina la mvulana huyo lilipotolewa mchezaji huyo alimtumia zawadi ikiwemo shati iliyopigwa saini kupitia shirika la umoja wa Mataifa ambalo anafanyia kazi kama balozi mwema.
Murtaza baadae alialikwa kukutana na Messi wakati nyota huyo wa Barcelona alipozuru Doha kwa mechi ya kirafiki mwaka 2016.
Kijana huyo mdogo aliondoka uwanjani na nyota wake wa kandanda anayemuenzi duniani.