- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : WANARIADHA 600 KAMBINI KUELEKEA ARGENTINA
Takribani wanariadha 600 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania wanatarajia kuanza mazoezi kujiandaa na mashindano ya Nyika kwa ajili ya kuwania nafasi ya kuunda timu ya Taifa ambayo itawakilisha katika michuano ya Afrika
Mashindano hayo ya kitaifa yataanza kutimua vumbi wiki mbili zijazo,katika hatua ya awali ya mchojo,ili kupata timu imara ambayo itasafiri moja kwa moja hadi Nchini Argentina,kuchuana na miongoni mwa wanariadha kutoka Nchi za Afrika
Rogath John ambaye ni katibu wa shirikisho la riadha mkoan Arusha,alisema mikoa yote ya Tanzania imethibitisha kupokea wanariadha wake,katika shauku hiyo ya kuwania nafasi ya kushiriki mbio za nyika,ambapo mchujo wa kwanza utaanza novemba 11
"Mbio zitafanyika katika uwanja wa magereza uliopo kisongo,nje kidogo ya jiji la Arusha,ambako ndio eneo zuri kwa ajili ya mashindano haya,ambapo pia taasisi za usalama zimethibitisha ushiriki wao ikiwemo Magereza "alisema Rogath John
Aliongeza kuwa mwaka huu kutakuwa na utofauti kulingana na kanuni za shirikisho la riadha duniani,kwa maana washindi watakaopewa zawadi ni kuanzia kwa kwanza hadi wa sita,tofauti na zamani,na zawadi zitatolewa kila upande kwa wanawake na wanaume