- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : WAAMUZI 220 WAJITOKEA DAR ES SALAAM KUPIMA UTIMAMU WAO
Zoezi la upimaji wa Utimamu wa waamuzi limendelea jana katika uwanja wa Taifa kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam ambapo baada ya kupimwa afya zao waamuzi hao watarajiwa wameanza kufanya mazoezi ya kukimbia yani ,Phyisical Test kabla ya kufanya semina maalumu siku ya jumamosi na kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa ajili ya kupata waamuzi watakaopewa beji ya fifa
Mazoezi hayo ambayo yalianza asubuhi uwanja wa taifa na kusimamiwa na mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Tanzania ambaye ndiye msimamizi, Israel Mkongo yaliendelea vyema mpaka jioni ambapo waamuzi takribani 220 wameshiriki katika kutafuta waamuzi ambao watapandishwa madaraja kutoka moja mpaka lingine
mazoezi ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Daraja la tatu na Pili kuwania kupanda, yafanyika katika vituo viwili Dar es salaam na mwanza,pia wale waamuzi wa Daraja la Kwanza walioshindwa mitihani hiyo mwezi Agosti, mwaka huu nao wamejumuishwa vyema kufanya mazoezi hayo pamoja na kufanya mitihani tena
katika kituo cha Dar es salaam waamuzi 220 wamejitokea kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na mitihani itakayowawezesha kutambulika na shirikisho la soka duniani Fifa kwa wale ambao watafaulu mitihani hiyo siku ya jumapili ya tarehe 15
Akizungumza makamu mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Tanzania Joseph Mapunda amesema waamuzi waliojitokeza ni 220 na baada ya kufaulu watapandishwa madaraja kama mbalimbali
Pia amesema miongoni mwa vigezo vilivyokuwa vikiangaliwa katika upimaji wa waamuzi hao,ni mapigo ya moyo ili wasije kuleta matatizo katika mazoezi ya kimwili ambayo yalifanyika uwanja taifa
"vigezo tulivyoangalia ni kwamba hatutaki kuona mtu akipata matatizo kwa hiyo moyo ndiyo kigezo kikubwa kilichoangaliwa sana"alisema Mapunda
Akiendelea kuzungumza zaidi makamu huyo amedai miongoni mwa waamuzi wanaowahitaji ni waamuzi wa ndani na pembeni,kwahiyo baada ya mtihani maalumu watakaofaulu ndiyo watakaokuwa na kazi hiyo kubwa,hata hivyo amesema suala la umri wamezingatia hivyo ni kuanzia miaka 18 na kuendelea
"Suala la Umri tumelizatia ni kuanzia miaka 18 na kuendelea ndiyo ambao tunawahitaji na sio tofauti"alisema makamu huyo mwenyekiti
Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Tanzania Isreal mkongo alifunguka na kudai mitihani watakayofanya ni mitatu siku ya jumapili,mtihani wa Offiside,Laws,na Match analysis
"Jumapili kutakuwa na mtihani wenyewe wa kufuzu kwa hawa maamuzi ambapo kutakuwa na mitihani mitatu,offiside,Laws na Match analyisis,atakayepita ataenda daraja lingine akitoka alipo"alisema mwenyekiti huyo"
Waamuzi 220 wamefanya mazoezi na kuonesha wapo tayari kuelekea mtihani utakaofanyika siku ya jumapili uwanja wa taifa kwa ajili ya kupandisha daraja waamuzi hao.