- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : TUNAFANYIA KAZI ENEO LA ULINZI-DANSON LIOBA
Baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Lipuli fc,timu ya Mbao fc imesema bado tatizo lao linaonekana kuwa ni sehemu ya ulinzi,ambayo mara zote imekuwa ikiwaangusha
Akizungumza na Muakilishi.com Msemaji wa Mbao fc,Danson Rioba amesema katika michezo kadhaa wamekuwa wakiongoza kipindi cha kwanza,lakini wanaporejea kipindi cha pili wamekuwa wakiruhusu mabao na hivyo kufungwa au kuambulia sare
Mbao fc ilikubali kipigo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Lipuli,huku tatizo kwa mbao likionekana kuwa ni sehemu ya ulinzi,baada ya kuongoza kipindi cha kwanza na mchezo huo kuisha kwa 2-1
Afisa Habari huyo pia amesema suala hilo linafanyiwa kazi na mwalimu wa timu hiyo,Ettiene Ndayiragijie huku akidai tayari wameandaa mikakati ya kuweka sawa sehemu ya ushambuliaji
"tunaanza na kuimarisha sehemu ya ulinzi ambayo mara kadhaa imekuwa na makosa yanayotugharimu,lakini tutaweka sawa sehemu ya ushambuliaji kuongeza kasi ya kufunga"alisema Danson Rioba
Katika mchezo uliochezwa wiki iliyopita Mbao fc ilikubali sare ya 2-2 baada ya kuongoza kipindi cha kwanza kwa magoli mawili kwa sifuri,lakini hali ilibadilika kipindi cha pili baada ya kujikuta wakiambulia sare
Rioba pia amesema kwa sasa wapo katika nafasi mbaya zaidi hivyo wamewasilisha maoni kwa mwalimu wa timu hiyo,na kuna kila sababu za kufanya juhudi na kujiondoa katika nafasi waliyopo kwa sasa
Mbao inashika nafasi ya kumi ikiwa na alama saba pekee,huku wakiwa wamefungwa michezo mitatu na kutoa sare michezo minne,wakati huohuo wameruhusu goli kumi na moja,na kufunga goli tisa,tofauti ikiwa ni goli mbili za kufungwa na kufunga.