- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : TANZANIA YAANZA VIBAYA MICHUANO YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YA MPIRA WA MIKONO
Timu ya mpira wa mikono ya Black Mamba kutoka Nchini kenya imeanza vyema kwenye michuano ya afrika mashariki na kati baada ya kupa ushindi dhidi JKT ya tanzania katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo uliofanyika leo jioni hii katika uwanja wa indoor taifa jijini Dar es salaam
Black Mamba imeifunga Jkt katika mchezo huo wa ufunguzi kwa jumla ya mabao 25 kwa 20,ambapo mpaka mapumziko timu ya JKT ilikuwa bado iko nyuma kwa mabao 13 kwa 10
JKT ilikuwa ya kwanza kufungua ukurasa wa mabao,na kuwapa moyo baadhi ya mashabiki,kuwa huenda ingeweza kuibuka na ushindi mpaka mwisho wa mchezo lakini,hali ya wapinzani wao ilikuwa vyema kuanzia mwanzo hadi mwisho
Katika mchezo huo makocha wa timu zote mbili walionekana wakitoa maelekezo zaidi ya kiukali kwa wachezaji wao,huku kila mmoja akihofia kupoteza mchezo wake wa kwanza
Kocha wa timu ya Black mamba,Abdallah Otelo amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini asilimia kubwa ya kile alichowaagiza wachezaji wake ndicho walichotekeleza na kutaja kuwa hiyo ndiyo siri ya ushindi wake wa kwanza
"Unajua sisi ni wageni hapa na tumeshinda mchezo wetu wa kwanza,nafikiri kile nilichowagiza wachezaji wangu ndicho kwa asilimia kadhaa walichotekeleza ndiyo maana tumeshinda"alisema Otelo
Kwa upande wake kocha wa timu ya Jkt amesema timu yake inawachezaji wengi ambao ni ingizo jipya kwa hiyo bado hawana uzoefu wa kutosha ndiyo maana walipoteza mchezo huo na kuahidi kufanya vyema kwenye mchezo ujao
Baada ya ushindi huo timu ya Black mamba ya kenya sasa inajiandaa na mchezo wake wa pili dhidi ya timu ya Polisi kutoka nchini Kongo utakaofanyika kesho saa 3:00 asubuhi