- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : SIMBA YAONGOZA KWA KUTOA WACHEZAJI WENGI TUZO ZA UCHEZAJI BORA
ACHANA na ubingwa wa Ligi Kuu, unaambiwa Simba ndiyo klabu pekee inayoongoza kwa kutoa wachezaji wengi zaidi kwenye kinyang'anyiro cha kuwania uchezaji bora wa mwaka 2017/2018 wa Ligi hiyo.
Mabingwa hao wapya wametoa wachezaji saba wanaowania tuzo hiyo, ikifuatiwa na Azam na Yanga ambazo kila moja imetoa wachezaji watano watano katika kinyanganyiro hicho.
Wakulima wa Alizeti,timu ya Singida United haijawa mbali sana kwenye hilo na imefanikiwa kutoa wachezaji watatu,huku wapinzani wao katika mchezo wa fainali ya kombe la TFF Mtibwa Sugar ikitoa wachezaji wawili wakati vilabu vingine mmoja na kukosa kabisa.
Nyota wa Simba waliongia kwenye tuzo hiyo ni golikipa Aishi Manula, mshambuliaji Emanuel Okwi na John Bocco viungo ni Jonas Mkude na Shiza Kichuya mabeki ni Asante Kwasi na Erasto Nyoni
Mabingwa wa kihistoria Ligi Kuu Bara Yanga wametoa watano ambao ni beki Kelvin Yondani na Gadiel Michael,viungo ni Ibrahim Ajibu na Mkongo Papy Tshishimbi na mshambuliaji Obrey Chirwa.
Kwa upande wa Azam FC ni Yahya Zayd, Razack Abarola, Aggrey Morris, Himid Mao, Bruce Kangwa na Singida United ni Shafiki Batambuze, Mudathir Yahya, Tafadzwa Kutinyu,wakati Mtibwa Sugar waliongia ni Shabani Nditi na Hassan Dilunga .
Wengine ni Habibu Kiyombo (Mbao), Hamis Mcha (Ruvu Shooting), Awesu Awesu (Mwadui), Adam Salamba (Lipuli) , Mohamed Rashid (Tanzania Prisons), Marcel Kaheza (Majimaji), Eliud Ambokile (Mbeya City) na Ditram Nchimbi (Njombe Mji).
Sherehe za utoaji wa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara 2017/18 zitafanyika Juni 23,2018 ambapo tuzo zingine pia zitatolewa.