- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : SIMBA WAKINIFUNGUZA NI SAFI TU YANI -OMOG
Siku kadhaa baada ya kuibuka kwa tetesi zikimuhusisha kocha wa Simba, Joseph Omog kuhusiana na kibarua chake kuwa matatani,hatimaye kocha huyo Mkameruni amefunguka kuhusiana na tetesi hizo
Siku za karibuni kumekuwa na uvumi mwingi juu ya simba kutaka kumtimua kocha huyo,kwa kushindwa kupanga kikosi chenye ushindani lakini,kocha huyo raia wa Kameruni amefunguka na kusema ikitokea akafukuzwa ni safi tu
Katika usajili wa dirisha kubwa uliofungwa Agosti 6, mwaka huu, Simba ilisajili wachezaji 14, hali ambayo inaifanya timu hiyo kuwa na nyota wengi wazuri akiwemo Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi. Licha ya kujaza nyota wengi kama hao, lakini Simba katika baadhi ya mechi imekuwa haipati matokeo ya kufurahisha jambo ambalo limetafsiriwa moja kwa moja kuwa Omog ameshindwa kukiongoza kikosi hicho
Wakati tetesi hizo zikizidi kuenea, Simba ilimleta nchini kocha Masoud Djuma raia wa Burundi ili awe msaidizi wa Omog baada ya kuondoka kwa Mganda, Jackson Mayanja, lakini imeelezwa kuwa, pindi Omog akiondoka, Mrundi huyo atachukua mikoba hiyo kwani alipokuwa akiinoa Rayon Sports kabla ya kutua Simba, alikuwa kocha mkuu
Akizungumzia mustakabali wake ndani ya Simba, Omog ameithibitishia Muakilishi.com kuwa yeye binafsi anaona anatakeleza kazi yake kwa ufasaha hivyo hana shaka hata kama watamfukuza
“Kwa sasa naona naifanya kazi yangu kwa ufasaha kwani ukiangalia msimamo tupo vizuri tu na wala si sehemu mbaya. “Makocha wengi wamekuwa wakitimuliwa kwenye timu zao, hivyo wala siho? i ikitokea jambo hilo kwa sababu naamini hakuna nilichoshindwa kukifanya, kama ushindi tunapata"alisema Omog
Hata hivyo mpaka sasa simba inaongoza ligi kuu bara ikiwa na alama 19 sawa na Azam,ikiwa ni tofauti ya magoli pekee,na mpaka sasa simba bado haijaonja ladha ya kufungwa katika mechi tisa walizocheza imeshinda michezo mitano na kutoa sare mara nne
Omog mwenye umri wa miaka 45 ,kabla ya kutua simba pia aliwahi kuifundisha Azam na kuipa ubingwa wa ligi kuu bara msimu wa 2013-2014,lakini pia aliwahi kuifundisha Fc Leorpad ya jamhuri ya Kongo,na ikumbukwe aliwahi kuchagulia kuwania tuzo za kocha bora wa shirikisho la soka barani afrika CAF