- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : SIMBA vs YANGA HAKUNA MBABE 0-0
Mchezo wa watani wa Jadi baina ya Simba na Yanga uliopigwa leo kwenye uwanja wa uhuru ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1 na mchezo huo kuisha sare mpaka dakika tisini
Mchezo huo uliokuwa mgumu wa aina yake haswa kwa namna ya timu zote kucheza kwa mfumo wa kujilinda zaidi ambapo mpaka mapumziko mchezo huo ulisha kwa sare ya tasa,bila kufungana
Makocha wa timu zote mbili walionekana kutopumua na kusimama wakitoa maelekezo kwa timu zao ingawaje hakuna timu iliyoibuka na ushindi
Kipindi cha pili kilianza kwa simba kushambulia huku ayanga wakionesha kujilinda zaidi,kutokana na umahili wa viungo wa simba,wakati mchezo huo ukiwa bado sare ya tasa mchezaji Shiza Ramadhani kichuya aliwasimamisha washabiki wa simba baada ya kutupia bao safi katika dakika ya 57 ya mchezo
Makosa ya mabeki wa simba Method Mwanjali na Juuko Mursheed,yalionekana wawagharimu dakika tatu baadae baada ya Mshambuliaji wa Yanga,Obrey Chirwa kuisawazishia timu yake ya yanga katika dakika ya 60 na mchezo kusomeka 1-1
Mchezo uliendelea kuwa wa kuvutia kwa namna ya umahili wa wachezaji wa timu zote mbili,ambapo kila timu ilikuwa inacheza kwa tahadhari ya kutoruhusu bao la pili,hali iliyopelekea mchezo huo kuisha kwa sare ya tasa
Mfungaji wa bao la simba Shiza Ramadhani Kichuya amesema wanashuruku kwa kupata alama moja na sasa wanaangalia mbele kwa ajili ya michezo mingine
"tunashukuru japo nimefunga bao likarudi mapema lakini ndio mchezo wa mpira ulivyo,kwasasa tunaangalia mbele kwa michezo mingine"alisema kichuya
Kwa upande wa Yanga mlinzi wa Pembeni Gadiel Michael amesema kuwa ni mara yake ya kwanza kwenye mchezo mkubwa kama huo,lakini wanashukuru kwa kupata alama moja ingawaje walipambana vyakutosha
"Nafikiri tulipambana vyakutosha tunashukuru kwa kupata alama moja ligi bado mbichi michezo ipo mingi kwahiyo huwezi kujua kitakachotokea baadae"alisema Gadiel
kikosi cha simba kilichoanza kwenye mchezo huo ni,Manula,Nyoni,Mohamedi
Hussein,Murushid,Mwanjale,Kotei,Yassin,Niyonzima,Kichuya,Mavugo,Okwi,wakati kwa upande wa Yanga kikosi kilichoaanza ni,Rostand,Abdul,Gadiel Michael,Vicent,Yondani,Tshishimbi,Buswita,Loth,Mwashiuya ,Chirwa,Ajibu
Baada ya mcheso huo kumalizika Timu ya simba ilijikuta inarejea Kileleni kwa alama 16,huku watani wao nao wakiwa na alama 16 kwa tofauti ya magoli na Azam wenye alama 16 pia,wakishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu tanzania bara.