- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : SIMBA KUANZA NA FAIR PLAY YA TANGA KATIKA KOMBE LA WANAWAKE
TIMU ya soka ya Simba Queens itafungua dimba na Fair Play ya Tanga katika Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Bara Novemba 27, mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Simba imepangwa Kundi A katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 26, mwaka huu chini ya udhamini wa Azam TV.
Simba imepangwa Kundi A mbalo mechi zake zitafanyika katika Kituo cha Dar es Salaam Uwanja wa Karume. Katika kundi hilo, Simba Queens iliyopanda daraja msimu huu ipo pamoja mabingwa watetezi, Mlandizi Queens, Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam na Fair Play ya Tanga.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.
Katika kundi hilo la A, mechi nyingine zitakuwa siku inayofuata Novemba 27, mwaka huu kati ya Mburahati Queens na Evergreen saaa 8.00 mchana wakati Fair Play ya Tanga itacheza na Simba Queens saa 10.00 jioni.
Jijini Arusha, Panama ya Iringa itafungua dimba na Alliance Queens ya Mwanza huku siku ya pili Novemba 27, mwaka huu Baobab Queens itacheza na Marsh Academy saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni Majengo Queens itapambana na Sisterz ya Kigoma.
Timu hizo zitapambana katika vituo hadi Desemba 12, mwaka huu kabla ya kutoa jumla ya timu nane kwa maana ya nne kutoka kila kundi. Timu hizo nane zitapambana katika hatua ya Nane Bora ya Ligi hiyo kuelekea ubingwa. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.