- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : SHOMARI KAPOMBE>MKATABA WANGU UKIVUNJWA SAFI TU
Baada ya mwenyekiti wa Klabu ya Simba Zakaria Hans Pope kumshushia lawama beki Shomari kapombe kuwa amepona majeraha yake yanayomkabili na anakaa nje kwa uoga wake huku akiendelea kula mshahara wa bure,hatimaye beki huyo ameibuka na kuzungumzia suala hilo
Beki huyo, tangu amejiunga na Simba msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwa dau la shilingi milioni 35, hajacheza mechi yoyote kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa na Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars
Mlinzi huyo wa zamani wa Azam amesema yeye bado mgonjwa na haogopi kucheza kama anavyoeleza Hans Poppe kwani hakuna kipya kitakachomuogopesha
Kapombe alisema, kwa mujibu wa daktari wake, atarejea uwanjani kucheza mechi za ligi kuu kwenye mzunguko wa pili akiwa imara kabisa
Aliongeza kuwa, kuhusiana na kuvunja mkataba wake, yeye hana tatizo kikubwa ni kufuata taratibu za kuuvunja hicho ndicho kitu cha msingi kwake
“Unajua mimi ninashindwa kuelewa, niliongea na Hans Poppe kwa njia ya simu na nikamuelezea tatizo langu, lakini nikashangaa kumsikia kwenye vyombo vya habari akinituhumu kuwa mimi siyo mgonjwa"alisema kapombe
Shomari Kapombe alienda mbali zaidi na kusema endapo suala la kuvunja mkataba wake likitoa basi yeye hana shida isipokuwa simba wafuate taaratibu za kuuvuja mkataba huo