Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 12:43 pm

SPORTS NEWS : SHOMARI KAPOMBE KUREJEA BAADA YA WIKI MOJA

Beki wa kulia wa Simba sc ameongezewa wiki moja zaidi mbele kutokana na majeraha aliyokuwa nayo ili kujimarisha zaidi pindi atakaporejea dimbani kwenye mechi za ligi kuu bara msimu huu

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amemuongezea wiki moja ya mapumziko beki huyo kisiki wa timu hiyo, Shomari Kapombe kabla ya kurejea uwanjani kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake

Akithibitisha kupewa mapumziko ya wiki moja Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema kwa mujibu wa ripoti ya daktari wao, Kapombe alitarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu wiki hii, lakini ameongezewa wiki moja ya kupumzika

"Kapombe amepona na yupo fiti kabisa kwa ajili ya mapambano na alitakiwa kuanza mazoezi Jumatatu ya wiki hii, lakini ameongezewa siku za mapumziko ili akirejea awe fiti zaidi,” alisema" Abbas Ally

Alisema beki huyo anatarajiwa kuanza tena mazoezi ya pamoja na wenzake wiki ijayo akiwa fiti kwa ajili ya kuendeleza mapambano,na kudai kuwa kurejea kwa beki huyo kutaimarisha kikosi hicho katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ili kuhakikisha wanashinda.

Beki huyo, alipata majeraha hayo ya nyonga akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na mechi dhidi ya Rwanda katika mechi ya marudiano kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani Chan.