Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:47 am

SPORTS NEWS : OBREY CHIRWA MCHEZAJI BORA MWEZI OKTOBA

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa amechaguliwa na shirikisho la shirikisho la soka Tff kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu tanzania Bara kwa msimu wa 2017-2018

Mzambia huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili,beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajibu pia wa Yanga ambao ndio alioingia katika kugombea tuzo hiyo kutokana na uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za ligi zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Tff kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha mbalimbali

Obrey Chirwa aliiwezesha timu yake kuvuna alama saba katika michezo mitatu na kuifanikishia kutoka nafasi ya sita mpaka ya pili kuanzia mwezi septemba mpaka oktoba mwishoni

Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambao umalizika kwa sare ya bao 1-1,huku bao la kusawazisha la Yanga likifungwa Obrey Chirwa

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa wa ligi kuu msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kwa mwezi ,Agosti, na beki wa Singida United, Shafiq Batambuze kwa mwezi Septemba