Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:39 am

SPORTS NEWS : NJOMBE MJI FC KUJIZATITI KWENYE USAJILI,ILI KUIMARISHA KIKOSI CHAO

Timu ya Njombe Mji imesema ipo katika mchakato wa kufanya usajili wanguvu ili kuimarisha sehemu mbalimbali ikiwemo nafasi ya ushambuliaji na beki wa kushoto,huku ikiwa na matumaini ya kufanya vyema katika michezo iliyobaki ya ligi kuu bara

Njombe Mji ambayo ipo katika nafasi ya kumi na tano ikiwa na alama saba,imesema pamoja na kufanya vibaya katika michezo ya ligi kuu,imejipanga kufanya usajili mkubwa ili iweze kujinasua na nafasi iliyopo katika michezo iliyobaki

Akizungumza na muakilishi.com Msemaji wa timu hiyo Solanus Mhagama,amesema watalazimika kufanya usajili ili kuzimba nafasi zenye mapungufu,kwa kuanza na nafasi ya ushambuliaji na nafasi ya ulinzi wa kushoto

Pia ameshindwa kuweka wazi wachezaji wanaowahitaji huku akidai kuwa wamepania kufanya usajili wa kimyakimya kutokana na baadhi ya timu kumuhitaji mchezaji fulani anapotakiwa na timu hiyo

"Usajili lazima tufanye wakimyakimya maana kuna timu zikisikia tunahitaji mchezaji na wenyewe wanamtaka pia,nafasi tuliyopo sio nzuri ila mechi bado nyingi nadhani tutafanya jambo"alisema Mhagama

Njombe Mji inashika nafasi ya 15 ikiwa na alama 7 pekee,huku ikiruhusu mabao 10 na kushinda mabao 3 tu,katika michezo yote 10 iliyochezwa kwenye ligi kuu tanzania bara

Hata hivyo kesho alfajiri timu hiyo itasafiri kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda sijaona siku ya Jumamosi novemba 25.