- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : NIYONZIMA AKIRI YANGA WALIMPANIA UWANJA WA UHURU
Kiungo Mchezeshaji wa Simba Mnyarwanda,Haruna Niyonzima amesema alikutana na ugumu dhidi ya timu yake ya zamani ya Yanga katika mchezo ulioisha sare ya 1-1 ,kutokana na wapinzani wake kumjua vilivyo
Mchezo wa Simba na Yanga ulichezwa wikiendi iliyopita katika dimba la uhuru ambao timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoa sare tasa ambayo ilifanya kila mmoja kujikuta akiwa na alama 16
Niyonzima amesema,mchezo ulikuwa na upinzani mkubwa hivyo anashukuru kwa matokeo waliyoyapata na kudai ilikuwa kazi kwa upande wake kutokana na kucheza na timu yake ya zamani ambayo inamjua vilivyo, lakini ataendelea kupambana kuisaidia timu yake
“Mechi ilikuwa na ushindani, kila upande ulikuwa ukipigana kuweza kupata pointi tatu, lakini tunashukuru kwa matokeo haya tuliyoyapata, tunaamini mwalimu atafanyia kazi upungufu uliojitokeza ili tuweze kufanya vyema katika mechi zijazo"alisema Haruna
Hata hivyo niyonzima alisema sio kazi rahisi kupambana na timu yake aliyoichezea kwa miaka mingi,kwani inamjua vilivyo ,ingawaje walimsumbua na kumkamia lakini bado alionesha ukomavu wa hali ya juu
“Mchezo ulikuwa mgumu,siyo kazi rahisi kwangu kupambana na timu niliyoichezea miaka mingi, pia wananifahamu, lakini nimejitahidi kucheza kulingana na jinsi hali ilivyokuwa, kwani nilikuwa na upinzani mkubwa, nilipambana kucheza katika kiwango kizuri kulingana na hali ilivyo ingawa walinisumbua sana,” aliongeza Niyonzima
Haruna niyonzima alisajiliwa akitokea Yanga baada ya kuitumikia kwa miaka mingi,na kuweka rikodi ya kuwa mchezaji wa kigeni ambaye amewahi kucheza soka kwa muda mrefu akiwa tanzania