Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:45 am

SPORTS NEWS : MKWASA ALALAMA TFF KUWAVURUGIA MIPANGO YAO

Siku Kadhaa kufutiwa shirikisho la soka Nchini Tff kusema Tanzania bara itashiriki michuano ya Chalenji itakayofanyika kenya,Uongozi wa klabu ya yanga kupitia kwa katibu mkuu wa timu hiyo Boniface Mkwasa amesema ratiba hiyo itavuruga mipango yao waliyojiwekea ya ligi kuu bara

Mashindano ya Chalenji yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi,Novemba 25 mwaka huu,ambapo hushirikisha timu za taifa za Nchi wanachama wa Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati Cecafa

Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema wao walikuwa wamejipanga kutokana na ratiba ya ligi kuu Tanzania bara,ambayo kimsingi ilikuwa haioneshi kama kuna mashindano ya chalenji

"Ligi inaposimama kila wakati kwakweli inatuvurugia mipango yetu,ambayo tulikuwa tumeiandaa kwa ajili ya kutetea ubingwa wetu"alisema Mkwasa

Mkwasa amesema Shirikisho la soka Tff ilipaswa kutoa taarifa mapema kama kutakuwa na mashindano ya Chalenji ili wapange ratiba zao wakijua kuwa tarehe fulani kutakuwa na michuano mingine


Kocha huyo wa zamani wa Taifa stars ameongeza kuwa wakati mashindano ya Chalenji yatakapofanyika ligi inapaswa kusimama kwa muda,hivyo kitendo hiko kinawavurugia ratiba zao pamoja na kuongeza gaharama za uendeshaji timu

"Wanavuruga mipango yetu,lakini pia wanatuongezea gharama za uendeshaji timu,kwa sababu ligi itakapokuwa imesimama basi,tutalazimika kuiweka timu kambini kwa muda mrefu kitu ambacho hakikuwa kwenye mipango yetu "alisema Boniface Mkwasa

Michuano hiyo itaanza Novemba 25 na kufikia tamati,disemba 9 mwaka huu,huku ikishirikisha timu za,Zanzibar,Uganda,Burundi,Kenya,Rwanda,Somalia,Sudani,Sudani Kusini Elitrea na Ethiopia.