- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : MKUTANO WA SIMBA WA KUMKABIDHI M DEWJI TIMU KUANZA MUDA HUU UKUMBI WA NYERERE KIGAMBONI
Siku moja baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom upande wa pili ni kuwa Mkutano Mkuu wa Mabadiliko ya Kikatiba wa Klabu ya Simba unatarajia kuanza hivi punde katika Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Simba ilikabidhiwa kombe hilo jana Jumamosi na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwenye Uwanja wa Taifa mara baada ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambapo Simba walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Klabu ya Simba inaenda kufanya mabadiliko hayo ya katiba maalum kuupokea mfumo mpya wa kisasa wa uendeshaji wa klabu hiyo.
Ikumbukwe Simba walitumia miaka takribani miwili kwa ajili ya mchakato wa mabadiliko na mwisho mshindi wa zabuni alipatikana ambaye ni Mwanachama na shabiki wa timu hiyo, Mfanyabiashara na bilionea Mohammed Dewji 'Mo'.
Mkutano huo unaenda kupokea rasmi mfumo huo mpya na wa kisasa kwa ajili ya klabu hiyo kujiwekeza zaidi kibiashara na kuachana na huu wa zamani unaotegemea ada za wanachama.