Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:41 am

SPORTS NEWS : LIONEL MESSI KAMA MCHAWI,AFANYA MAMBO YA AJABU

Kama ni Uchawi basi Messi ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,hana makamu! habari ndiyo hiyo

-Apiga hatrick ugenini na kuzama Urusi wanasema Simply the best

-Achukua mchezaji bora wa mechi hiyo

-Ufalme ni zaidi ya Maradona

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi usiku wa jana umefunga mabao matatu ‘hat-trick’ dhidi ya Ecuador nahivyo kuiwezesha timu yake kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi.

Katika mchezo huo Argentina wametoka nyuma wakiwa ugenini na kupata ushindi wa mabao 3-1 huku nyota huyo Messi akifunga mabao hayo na kujihakikishia kufuzu kombe la dunia.

Argentina sasa inaungana na Brazili,Uruguay na Colombia kuelekea nchini Urusi hapo mwakani.

Luis Suarez ametupia mara mbili wakati timu yake ya Uruguay ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bolivia na hivyo kukata tike ya kufuzu huku suluhu waliyo ipata timu ya taifa ya Colombia ya mabao 1-1 dhidi ya Peru imewafanya nao kuwa miongoni mwa timu hizo zitakazo shuhudiwa huko Urusi.

Peru iliyomaliza nafasi ya tano huko Amerika Kusini italazimika kusubiri mchezo wa ‘play-off’ dhidi ya New Zealand wakati mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez hatutamuona katika michuano hiyo baada ya timu yake ya taifa ya Chile kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Brazili.

Kikosi cha Ecuador: Banguera (6), Velasco (6), Renato Ibarra (7), Romario Ibarra (6), Jose Cevallos (6), Ordonez (6), Arboleda (6), Ramirez (6), Intraigo (6), Orejuela (6), Aimar (6)

Waliyokuwa benchi: Uchuariat (6), Valencia (6), Estradaat (6)

Kikosi cha Argentina: Romero (6), Mercado (6), Mascheraho (6) , Otamendi (7), Salvio (6), Perez (6), Biglia (6), Acuna (6), Messi (10), Di María (8), Benedetto (6).

Waliyokuwa benchi: Icardi (6), Fazio (6)

Lionel Messi amekuwa mchezaji bora wa mchezo huo ‘Man of the match’.