- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : KUWAFUNGA YANGA INATOKEA TU BAHATI-KICHUYA
Kiungo Mshambuliaji wa Simba,Shiza Ramadhani Kichuya,amesema kitendo cha kuwafunga wapinzani wao Yanga,kila wanapokutana kinatokea tu kwa uwezo wa Mungu lakini mwenyewe huwa hategemei kama atawafunga wanapokutana
Kichuya amezungumza hayo baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya watani wao wa jadi ulioisha kwa sare ya 1-1 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam siku ya jumamosi
Kiungo huyo mara kadhaa amekuwa akiwafunga yanga katika michezo ya ligi kuu tanzania bara,ambapo katika mchezo ulioisha sare uwanja wa uhuru,Kichuya amesema kitendo cha kuwafunga yanga hakutemegea ila inatokea tu kwa uwezo wa Mungu
"Sio kwamba nasema leo nitawafunga Yanga hapana,bali ni suala ambalo linatokea tu lenyewe bila kutarajia kwa uwezo tu wa mungu"alisema Kichuya
Katika Mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu uliopita Kichuya aliifunga yanga kwa Kuisawazishia katika dakika za mwisho kwa kona iliyoingia wavuni moja kwa moja,katika ushindi wa 2-1 walioupata simba mzunguko wa pili kichuya akaweza kufunga tena bao la ushindi
Katika mchezo wa mzunguko wa Kwanza uliopigwa oktoba 1 ,2016 kichuya alifunga bao la kona lililoisawazishia Simba na mchezo kuisha sare ya 1-1,katika mzunguko wa pili Yanga ililala 2-1 bao la simba la ushindi lilifungwa na kichuya
Kiungo huyo jumamosi akiwa uwanja wa uhuru dhidi ya Yanga kwa mara ingine akaifunga Yanga katika dakika ya 57 na kuipa simba bao la kuongoza,ingawaje bao hilo halikuweza kudumu,ambapo dakika tatu baadae bao hilo lilichomolewa na Mshambuliaji Obrey Chilwa
Kichuya akiwa na Simba,mpaka sasa ameshaifunga Yanga jumla ya magoli matatu katika michezo iliyopigwa ya ligi kuu tanzania bara katika michezo hiyo simba imeshinda mmoja na kutoa sare michezo miwili ukiwemo mchezo wa jana