- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : KOCHA MPYA WA VIJANA AZAM FC AWEKA MIKAKATI MIPYA
Kocha mpya wa timu ya vijana ya Azam FC chini ya umri wa miaka ishirini ,Meja Mstaafu Abdul Mingange,amesema moja ya mikakati yake ni kuifanya timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali pamoja na kupandisha wachezaji watakaoongeza nguvu katika timu kubwa
Abdul Mingange,aliwahi kuzifundisha timu za Ndanda na Tanzania Prisons,jana alitangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho akichukua mikoba ya kocha wa muda mrefu wa timu hiyo, Idd Nassor Cheche, ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa tangu mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana
Akizungumza na kwenye mahojiano maalumu kocha huyo alisema kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili ijayo,timu hiyo itakuwa na mtazamo tofauti chini yake tofauti na ilivyo sasa huku akiweka wazi kushirikiana na watangulizi wake waliokuwa wakikinoa kikosi hicho
“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata bahati ya kuja kuwepo kwenye timu ya Azam FC hasa kwenye timu ya vijana kwa sababu mimi napenda sana kufundisha vijana na nilishafanya hivyo miaka iliyopita"alisema Mingange
Pia amesema lengo lake kubwa kuhakikisha baadhi ya wachezaji vijana wanapandishwa kwenye timu ya wakubwa ili kuleta nguvu mpya kwenye kikosi cha Azam ambacho kinashiriki ligi kuu tanzania bara
"nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuhakikisha timu yetu ya vijana infanya vizuri na tunaweza kupandisha vijana wakeongeza nguvu kwenye timu yetu kubwa,” alisema Mingange
Azam imekuwa na mfumo wa utumiaji wa wachezaji vijana kwenye timu za wakubwa kwani hata,mwalimu Aristica Cioaba ameanza kuwa na utamaduni wa kuwaamini na kuwatumia wachezaji vijana ambao mara zote hawamuangushi
Hata hivyo mfumo wa utumiaji wa wachezaji vijana umekuwa ukipingwa na baadhi ya mashabiki wa azam wakidai ndio sababu ya kutofanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu tanzania bara.