Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:42 pm

SPORTS NEWS : IDDI CHECHE,MBEYA CITY NI SHIDA KIDOGO

Kocha Msaidizi wa Azam fc Iddi Nassoro Cheche amesema pamoja na kuibuka na Ushindi katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa siku ya ijumaa,kulikuwa na upinzani wa kutosha na kusifu kiwango cha Mbeya city walichokionesha katika mchezo huo

Azam ikiwa katika uwanja wao wa Nyumbani iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kuwapa alama tatu muhimu na kufanya kuongoza ligi kwa muda kabla ya mchezo wa watani wa jadi uliopigwa jumamosi,ambao umewashusha azam mpaka nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli

Cheche amesema kuwa mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho huku akidokeza kwamba kama mechi zote za ligi zingekuwa zikichezwa kwa kiwango hicho basi soka la Tanzania lingepiga hatua nzuri

“Nafurahi kwa ushindi na vile vile nafurahi kwa kiwango na ushindani tuliokutana nao katika mechi, kama tunakuwa tunacheza ligi katika mechi zote kwa namna hii nafikiri kiwango chetu cha mpira Tanzania kingekwenda juu, lakini inatokezea baadhi ya mechi moja moja mechi nyingi zinakuwa na matatizo,” alisema Iddi Cheche

Bao pekee lililoipa Azam alama tatu, lilifungwa na Mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi Septemba-Oktoba,mshambuliaji Mbaraka Yusuph, akitumia vema kona iliyochongwa na winga Enock Atta na mpira kumgonga mgongoni baada ya kumponyoka kipa wa Mbeya City, Owen Chaima

Azam sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 16 sawa na simba na yanga,ikiwa ni tofauti ya magoli pekee kwenye msimamo wa ligi kuu bara wa mzunguko wa nane.