Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:49 am

SPORTS NEWS : HARUNA NIYONZIMA KUTIMKIA RWANDA BAADA YA MCHEZO DHIDI YA LIPULI JUMAPILI HII

Kiungo wa Simba sc Haruna Niyonzima amesema anatarajia kuondoka kwenda nchini kwao Rwanda,baada ya mchezo wa jumapili dhidi ya Lipuli fc utakaopigwa kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam

Niyonzima amesema baada ya mchezo huo wa jumapili ataondoka kwenda nyumbani kwao Rwanda kwa ajili ya kuhani misiba ya ndugu zake ukiwemo msiba wa aliyekuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya,Hamad Ndikumana

Hamad Ndikumana alifariki dunia novemba 15 mwaka huu,wakati kiungo Haruna Niyonzima akiwa kwenye majukumu ya klabu yake ya simba mkoani Mbeya,amesema alitakiwa kuondoka jana Jumanne lakini hakuweza hivyo hadi ahakikishe anamaliza mchezo wao dhidi ya Lipuli fc,ili aweze kuondoka vizuri kwani alipatwa na misiba takribani mitatu

Kabla ya msiba wa Hamad Ndikumana,kiungo Haruna Niyonzima alifiwa na mama yake mlezi,hivyo hakuweza pia kuhudhuria kutokana na majukumu ya klabu yake,wakati simba ilipovaana na Mbeya city

"Nilitakiwa jana jumanne niende Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria kwenye misiba mitatu iliyotokea nikiwa Mbeya kwenye majukumu ya klabu yetu, kama unakumbuka kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City nilifiwa na mama yangu mlezi"alisema Niyonzima

Baada ya msiba huo wa mama yake Mlezi,Kiungo huyo alisema,alijisikia vibaya baada ya kupata taarifa za misiba mingine miwili ya ndugu yake,Hamad Ndikumana na mchezaji mwenzie wa taifa la Rwanda,hivyo hana jinsi lazima aondoke baada ya mchezo wa jumapili

“Lakini pia siku chache kabla ya kukutana na Prisons, nilipata misiba miwili tena ambapo ndugu yangu kabisa Hamad Ndikumana alifariki dunia pamoja na mchezji mwezangu wa timu ya taifa alifariki jambo ambalo kwa namna moja au nyingine limeniuma hivyo lazima niende,”aliongeza Niyonzima

Mchezaji huyo ataondoka tanzania kwenda nchini kwao baada ya mchezo wa Lipuli fc,siku ya jumapili ingawaje hakuweka wazi ni siku gani baada ya mchezo huo ataondoka.