- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : HARUNA NIYONZIMA AMKINGIA KIFUA LAUDIT MAVUGO
WAKATI tetesi za kutemwa kwa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kukosa timu kama akiachwa.
Mavugo ni kati ya wachezaji waliopo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo la msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile kinachotajwa kiwango chake kushuka.
Mrundi huyo, tayari ameanza kunyatiwa na baadhi ya klabu za nje ya nchi na kati ya hizo ni Gor Mahia ya Kenya. Niyonzima alisema Mavugo bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, lakini vitu vidogo ndiyo vinamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake.
Niyonzima aliongeza, mshambuliaji huyo kinachomfanya ashindwe kucheza ni presha kubwa iliyopo kwenye timu huku akimtabiria kuwa akienda kwingine atacheza vizuri.
“Mavugo siyo mbaya kiasi hicho, binafsi naona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika timu.Lakini kitu kikubwa kinachomfanya ashindwe kucheza vizuri ni presha iliyopo katika timu pekee na siyo kitu kingine Ninakuhakikishia akienda timu nyingine tofauti na Simba atakuwa tegemeo, kwani ana uwezo mkubwa,” alisema Niyonzima."alisema