- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : ERIC BAKAME ACHIMBA MKWARA MZITO,KUELEKEA MICHUANO YA CHALENJI DESEMBA 3
Nahodha wa kikosi cha Rwanda kitakachoshiriki michuano ya CHAN mwakani nchini Morocco, Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye amesema kuwa michuano ya Kombe la Chalenji itatoa picha halisi kwa taifa hilo kuelekea kwenye fainali za Kombe CHAN mwakani.
Rwanda, maarufu kama Amavubi wamepangwa Kundi A ambapo zipo pia timu za Tanzania na Zanzibar na waalikwa kwenye michuano hiyo, Libya ambao nao wanataraji kuitumia michuano hio kama sehemu ya maandalizi kuelekea kwenye michuano ya CHAN.
“Michuano ya Kombe la Chalenji itatuonesha picha halisi juu ya kile tutakachokwenda kukifanya kwenye michuano ya CHAN, tunataka kwenda kushinda michezo yetu yote kwenye Kombe la Chalenji kitu ambacho kitatupatia morali kubwa kuelekea kwenye CHAN,” alisema.
Nahodha huyo aliongeza kuwa kupangwa kwenye kundi moja na Libya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji kutawasaidia kuwasoma wapinzani wao hao kwani wapo kwenye kundi moja pia kwenye Kombe la CHAN.
“Tupo kwenye kundi moja na Libya kwenye Kombe la Chelenji na CHAN, hio itatusaidia sana kufahamu namna ya uchezaji wao,”
Rwanda itacheza mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Chalenji dhidi ya Kenya ambao ndio waandaaji wa michuano hio inayotarajiwa kuanza Disemba 3 hadi 17.