- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : AZAM YAWASILI NJOMBE,MCHEZO WAO WASOGEZWA MBELE MPAKA JUMAPILI
Msafara wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, umewasili salama mkoani Njombe jana jioni, ukiwa tayari kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na Njombe Mji katika mchezo wa raundi ya 10 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
Azam FC imetumia takribani saa 15 kuwasili mkoani humo, ambapo kilianza safari jijini Dar es Salaam saa 10 alfajiri.
Wakati kikosi hicho kikiwasili, taarifa kutoka Bodi ya Ligi hiyo, inaeleza kuwa mchezo kati ya wenyeji Njombe Mji na Azam FC, uliotarajiwa kufanyika Jumamosi hii umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Jumapili.
Mchezo huo umesogezwa mbele ili kuwapa nafasi wadhamini wa matangazo ya televisheni, Kampuni ya Azam Media kupitia luninga yao ya Azam TV, kurusha mbashara mpambano huo.
Kikosi hicho kipo kwenye hali nzuri kabisa kuelekea mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake, ambapo kitawakosa nyota wake watatu mabeki Daniel Amoah, Yakubu Mohammed na nahodha Himid Mao ‘Ninja’, ambao kila mmoja amekusanya kadi tatu za njano.