- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : AZAM FC YATUMA SALAMU KWA RUVU SHOOTING,YAINYUKA ASHANTI 4-0
Azam fc imewatumia salamu Ruvu shooting,katika mchezo utakaopigwa wikiendi hii,baada ya kuwanyuka Ashanti United Goli nne kwa bila,katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku wa kuamkia jana,uwanja wa Azam Complex Chamazi
Mtanange huo uliokuwa na lengo la kuwaweka kwenye ushindani wachezaji, pia wakipasha misuli kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika uwanja wa azam complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku
Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii msimu uliopita walijipatia mabao mawili katika kila kipindi, ambapo winga Enock Atta, aliyeendelea kuwa kwenye kiwango chake kizuri alifunga bao la uongozi dakika ya nane baada ya kuitoka safu ya ulinzi ya Ashanti na kupiga shuti lililojaa wavuni
Kiungo wa pembeni Idd Kipagwile, aliipatia azam bao la pili dakika ya 31 ,na hivyo kufanya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika kwa uongozi wa mabao mawili ya Azam fc huku Ashanti wakiwa hawajapata kitu
Kipindi cha pili Azam FC ilihitimisha ushindi huo mnono kwa mabao mengine mawili, yaliyofungwa na mshambuliaji Wazir Junior dakika ya 75 na jingine likiwekwa kimiani kwa mkwaju wa penalti na beki David Mwantika dakika ya 86
Kiungo Salmin Hoza, alionekana kuwa ni moto kwenye mchezo huo ambapo angeweza kuipatia mabao mengine mawili Azam FC baada ya mashuti yake mawili aliyopiga kugonga mwamba
Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kimeingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting, utakaofanyika wikiendi hii katika dimba lao la nyumbani Azam Complex.