Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 2:34 pm

SPORTS NEWS : ARISTICA CIOABA -KUPATA USHINDI UGENINI SIO MCHEZO


Baada ya kuambulia sare ya 1-1 na Mwadui fc ,huko mkoani Shinyanga benchi la ufundi la timu ya Azam limeweka wazi kuwa sio kazi rahisi kupata matokeo ya ushindi wakiwa ugenini,kwani kuna hali ya baadhi ya timu za mikoani kukamia michezo hiyo

Azam ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga,ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi wenyeji wao Mwadui katika dimba la Mwadui Complex mkoani Shinyanga siku ya jumamosi

Kocha wa Azam Aristica Cioaba amesema,walijiandaa vizuri,lakini ukamiaji wa timu ya Mwadui ndicho kilichowafanya kuondoka na Alama moja pekee katika dimba la Mwadui Complex

“Huku mikoani kugumu sana kupata alama,nasema hivyo kwa sababu tunaocheza nao mara nyingi wanajitoa kupigania wasifungwe na kupoteza alama kwenye kiwanja chao cha nyumbani, jambo ambalo huwafanya wacheze kwa ustadi wa hali ya juu"alisema Aristica Cioaba

Pia amesema kwasasa wao wanachoangalia ni mchezo ujao kwani mechi hiyo imeshapita,hivyo wameyapokea matokeo hayo kwa namna yote,sasa wanaangalia mechi zijazo kwa ajili ya kufanya vyema

“Lakini hata hivyo siyo mbaya kuambulia pointi hii moja tuliyoipata ambayo inatufanya tuendelee na mapambano yetu mengine kwenye ligi, na kuhusu mchezo huu tayari tumeshaumaliza, tunachokiangalia kwa sasa ni juu ya michezo yetu ijayo,” aliongeza kocha huyo

Mpaka sasa Azam imefikisha alama 11 sawa na Mtibwa Sugar na Simba,yenyewe ikishika nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli ,Azam itasafiri kuelekea mkoani Mwanza kukipiga na Mbao fc katika dimba la Ccm Kirumba siku ya jumamosi Oktoba 21 mwaka huu

Benchi la Ufundi la Azam chini ya Mromania Aristica Cioaba ,wamewaka bayana kuwa