- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : ARISTICA CIOABA KUENDELEA KUWATUMIA VIAJANA
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuungana naye katika kuwapa moyo wachezaji vijana ambao anaendelea kuwaamini na kuwapa nafasi katika kikosi cha kwanza
Timu ya Azam msimu huu imekuwa ikiwatumia wachezaji wengi vijana huku katika eneo la ushambuliaji ikiwa na changamoto kubwa kutokana na kuwa na wachezaji wengi vijana wanacheza kwa pamoja ambao wanahitaji muda mwingi kuweza kuimarika vyema
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na walitoka sare ya tatu mfululizo kwenye mechi za ugenini za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Mbao,katika uwanja wa ccm kirumba siku ya jymamosi ,mechi nyingine mbili za nyuma zikiwa dhidi ya Mwadui 1-1 na Singida United 1-1
Kocha Cioaba ameweka bayana kuwa amepanga kuwapa nafasi wachezaji vijana licha ya maneno mengi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo,na anaamini ya kuwa muda si mrefu watawapa mashabiki kile ambacho wanahitaji kutoka kwao cha muhimu ni kuwaunga mkono wa kuwapa muda
“kwenye mechi na Mbao tulipata nafasi lakini tumeshindwa kuzitumia ,mashabiki wanatakiwa kutambua ya kuwa kwenye mechi na Mbao niliweza kuchezesha wachezaji wengi vijana, Razak ana miaka 20, Daniel 20, Yakubu 22, Enock 19, Idd 20, Zayd 20, Mbaraka ana miaka 21,alisema Cioaba
Pia amesema watu wanatakiwa kutambua wachezaji wengi vijana hawana uzoefu,hivyo kazi iliyobaki ni kuwajenga ili kuapata uzoefu wa kutosha na kuwa na makali zaidi katika siku zijazo
“Wachezaji wengi ni vijana na wengi hawana uzoefu, wachezaji hawa wanahitaji hali ya kujiamini ili kuweza kufanya vizuri, mashabiki waendelee kuwaamini, mechi imeisha kwa sare na lengo letu lilikuwa ni kuchukua pointi tatu, hivyo tutafanya kazi kubwa kuzidi kuwajenga hawa wachezaji vijana ili kuweza kuwa na makali kwenye ushambuliaji,” alisema Aristica Cioaba
Kocha huyo alisema licha ya kuwa na wachezaji wengi vijana, bado kikosi chake kimekuwa na mwenendo mzuri kwenye mechi saba za mwanzo walizocheza, ambapo hawajapoteza mchezo hata mmoja
“Sisi tumejikusanyia pointi 13, waliokuwa juu yetu Simba, Yanga na Mtibwa Sugar wametuzidi pointi mbili tu, si jambo baya, tutaendelea kufanya kazi zaidi ya kukiboresha kikosi ili kuwa imara zaidi, cha muhimu ni mashabiki nao kuisapoti timu na kukaa karibu na wachezaji vijana kwa kuwapa moyo na kuwasapoti na hatua kwa hatua mabao yatakuja,” aliongeza kocha huyo
Aidha alisema kuelekea mchezo ujao dhidi ya Mbeya City, wataingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mtanange huo unoatarajia kupigwa Ijumaa ijayo Oktoba 27 mwaka huu.