Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:58 am

SPORTS: KROENKE ATANGAZA OFA YA KUINUNUA ARSENAL KWA ALISHER

London: Bilionea Mmarekani, na mmiliki wa club ya Arsenal Stan Kroenke ametoa ofa ya euro Bilioni £1.8 ili kununua asilimia 30 ya hisa za Alisher Usmanov katika klabu ya Arsenal, ili kuimiliki rasmi klabu hiyo kwa asilimia 100%

Kroenke kwa sasa anamiliki asilimia 67 ya hisa kupitia kampuni yake ya Kroenke Sports Enterprise group (KSE),

Taarifa KSE inasema kuwa kuichukua club hiyo na kuifanya kuwa binafsi "itasaidia club ya Arsenal katika mikakati na malengo ya club"

Taarifa ya kununua imetanganzwa leo Jumanne kwenye soko la hisa la london licha ya usmanov kutokuwa sehemu ya bodi ya wakurungezi kwenye club hiyo.

Taarifa kwenye soko la hisa la london inaongeza kuwa" malengo ya KSE kwa club ni kuona Arsenal inashindana katika kushindania Mataji makubwa likiwemo la Ligi na Champions league vile vile hata mataji mengine makubwa katika upande wa wanawake na vijana"