- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: JOB NDUGAI MGENI RASMI MCHEZO WA SIMBA NA YANGA
Dar es salaam: SHIRIKISHO la Kabumbu Nchini Tanzania (TFF) jana Limemtangaza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) unao wakutanisha watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.
Simba na Yanga zinakutana leo Sept. 30 katika mchezo wa Ligi kuu kuanzia majira ya saa 11 jioni ukiwa ni mchezo uliosubiriwa kwa ham na mashabiki na Wadau wa Michezo Tanzania
Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa jana kupitia mtandao wa Shirikisho hilo wakimtangaza Mhe. Job Ndugai kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo ya watani wa jadi huku viongozi mbalimbali nao wakitarajia kuja kushuhudia mchezo huo.
Simba na Yanga zinakutana katika Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa ni mara ya 93, Yanga akishinda mara 34 na Simba mara 26 huku wakitoka sare mara 30.Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini utakuwa wa kusisimua kwa kila upande kutaka kuibuka na ushindi.
Mitaani kumekuwa na tambo mbalimbali kutoka kwa mashabiki, kila upande wakisifia kikosi chao kwa upande wa Simba wenye alama 10 baada ya kucheza mechi 5 watashuka dimbani bila mshambuliaji wao John Bocco anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu lakini wakiwa na washambuliaji wengine Kama Meddie Kagere, Emanuel Okwi, Marcelo Kaheza na Adam Salama.