Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:48 pm

SPORTS: BARCELONA YAKANUSHA KUVUNJA SHERIA ZA USAJILI KWA RABIOT WA PSG

Club ya Barcelona imetoa taarifa jioni ya leo ikikanusha kuwepo kwa taarifa ya club hiyo kuvunja sheria za usajili kwa kumsaini kiungo wa club ya Paris Saint Germen Adrien Rabiot.

Rabiot mkataba wake na PSG Unakwisha katika majira ya joto mwakani, hii ikimanisha kuwa kiungo huyo anauwezo wa kufanya mazungumzo na club yeyote kwaajili ya kuitumikia kwa msimu ujao katika dirisha la usajili mwezi January.

Rabiot '23' alikuwa anahusishwa na club za Ligi ya Uingereza Arsenal na Liverpool lakini taarifa zilizopo ni kwamba Rabiot ameshafanya makubaliano na miamba ya soka ya Uhispania Fc Barcelona.

Ingawa Barcelona imetoa taarifa kusema kuwa " ieleweke kuwa hatujavunja sheria yeyote ya usajili" ilisema sehemu ya taarifa.