- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: ZLATAN AWAFIKIA KWA MABAO WACHAWI MESSI NA RONALDO
Hatimaye Mchezaji wa kulipwa wa club ya LA Galaxy ya nchini Marekani Zlatan Ibrahimovic ameungana na wachawi wa soka wa dunia Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuwa miongoni mwa wachezaji ambao bado wanacheza katika sayari hii waliofunga mabao 500 na zaidi wakichezea timu kubwa ya klabu na taifa.
Zlatan amefikisha rekodi hiyo baada ya kufunga bao la kushangaza dhidi ya Toronto nchini Marekani.
Club yake ya LA Galaxy ilikuwa nyuma 3-0 kabla ya mapumziko, lakini mshambuliaji huyo wa Sweden aliupiga mpira kwa kisigino cha mguu wake ukiwa ungali hewani na kuutumbukiza wavuni.
Bao lake hata hivyo halikuwasaidia LA Galaxy kwani Toronto mwishowe waliibuka washindi wa 5-3.
"Nawafurahia Toronto kwa sababu watakumbukwa kama waathiriwa wangu wa 500," Ibrahimovic aliambia runinga ya TSN baada ya mechi hiyo.
Lilikuwa ni bao la 17 kwa Ibrahimovic kuwafungia LA Galaxy tangu ajiunge nao kutoka Manchester United mwezi Machi mwaka huu.
Kwa sasa, ndiye mfungaji mabao bora wa Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na Canada (MLS) msimu huu.
Ibrahimovic, 36, amecheza mechi 747 za ushindani.
Amefunga jumla ya mabao 438 akichezea Malmo, Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, Paris St-Germain, United na LA Galaxy.
Mabao 62 ameyafunga katika mechi 114 za kimataifa alizochezea taifa lake la Sweden.
MABAO ALIYOFUNGA
Malmo (1999-2001) - 18
Ajax (2001-2005) - 48
Juventus (2004-2006) - 26
Inter Milan (2006-2009) - 66
Barcelona (2009-2010) - 22
AC Milan (2010-2012) - 56
PSG (2012-2016) - 156
Manchester United (2016-2018) - 29
LA Galaxy (2018-present) - 17
Sweden (2001-2016) - 62