Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:38 pm

SPORT: YAFAHAMU MAKOSA 2 YAKUFUNGIWA MENEJA WA SIMBA

Dar es salaam: KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF) kupitia mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni Jana limemfungia Meneja wa wekundu wa msimbazi Simba sport club, Robert Richard kutojihusisha kabisa na maswala ya soka kwa kipindi cha mwaka mzima na faini ya shilingi milioni 4, baada ya kukutwa na makosa mawili ya kimaadili.

Meneja wa Simba, Robert Richard

Kosa la kwanza la meneja huyo ni kuhujumu timu ya Taifa kwa kutotii wito wa TFF na kosa la pili kuchelewesha kuwapa taarifa kwa wakati wachezaji wa Simba kujiunga na timu ya Taifa ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Afrika dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliwaondoa kwenye kikosi wachezaji sita wa kikosi cha Simba kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini katika muda muafaka.

Wachezaji hao ni Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Shomari Kapombe, John Bocco, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni.

Meneja huyo kuanzia sasa hatoonekana kwenye benchi la klabu ya Simba kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na hata ile ya klabu bingwa barani Afrika kutokana na kuwepo kifunguni kwa mwaka mzima.