- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: HATIMAYE SIMBA WAMSAJILI BEKI WA LIPULI ASANTE KWASI
Dar es salaam: Klabu ya Lipuli FC, ya Iringa, imekubali kumuachia beki wake Asante Kwasi, kujiunga na Simba, baada ya awali kugomea usajili huo ukidai Simba hawajafuata utaratibu maalumu unaotakikana.
Msemaji wa Lipuli Clement Sanga, ameiambia muakilishi.com, tayari wamemalizana na Simba na wameliandikia shirikisho la soka barua ya kuthibitisha kuwa mchezaji huyo hupo huru kujiunga na Simba ya Dar es Salaam.
"Kuanzia jana Kwasi ni mali ya Simba, kama uongozi tumeshamalizana na timu hiyo na tunamtakia kila la kheri huko anapokwenda pia tunamshukuru kwa kazi nzuri ambayo ameifanya akiwa anaichezea timu yetu,"amesema Sanga.
Usajili wa Kwasi ulileta utata mkubwa klabu ya Lipuli, ikigoma kumuachia kutokana na uongozo wa Simba kutumia nia za panya kumrubuni mchezaji huyoo na kumsajilisha siku ya mwisho ya pazi la usajili kufungwa.
Klabu yake iliandika barua ya malalamiko kwa TFF, ikipinga usajili huo lakini baada ya kutokea itilafu ya kimtandao hatimaye Shirikisho la soka liliongeza siku za usajili na Simba kufuata taratibu zinazotakiwa.
Kwasi anakwenda kuchukua nafasi ya Mzimbabwe, beki wa kati, Method Mwanjali ambaye ameachwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe.