Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:53 pm

SPORT NEWS: AHADI 10 ZA TAJIRI MO KWA SIMBA BAADA YA KUPEWA TIMU

  • Dar es salaam: Mkurugezi mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises (MeLT) Mohamed Dewji leo Tarehe 3 December 2017 amefanikiwa kushinda zabuni(tender) ya umiliki wa Club ya Simba sc kwa uwekezaji wa Tsh bilion 20. Dewji amefanikiwa kushinda Zabuni hiyo baada ya wajumbe wa kamati kuu ya simba kwa pamoja kumchagua Tajiri huyo, akimtangaza Mshindi wa zabuni hiyo Mwenyekiti wa kamati ya zabuni, Jaji Thoma Mihayo alisema kuwa kamati imemteua Mohamed Dawji kuwekeza katika club ya simba

"Oktoba 18, kamati maalum ya uwekezaji ilipokea maombi ya watu waliojitokeza kuwekeza SimbaSC Kamati ilikaa na kutathimini vigezo vilivyowekwa," Mwenyekiti wa kamati ya zabuni, Mwaliko kwa mwekezaji wa SimbaSC aliyekidhi vigezo ulitolewa mwezi wa kumi mwishoni ambapo Kamati imemteua moodewji kuwekeza katika klabu ya SimbaSCTanzania kiasi cha shilingi bilioni 20" Mwenyekiti wa kamati ya zabuni, Jaji Thoma Mihayo


Naye kwa upande wake Mo Dewji baada ya kangzwa kuwa mshindi wa zabuni hiyo alisema kuwa Wakati zoezi hili likifanywa na kamati, mengi yalizungumzwa ambayo hayakuwa na afya kwa klabu ya SimbaSCTanzania, " "Huu si ushindi wa moodewji, huu mi ushindi wa SimbaSCTanzania. sidhani kama kuna aliye na shaka juu ya ushabiki wangu juu ya SimbaSCTanzania "


baada ya maneno hayo Dewji akaahidi ahadi 10 kama ifwatavyo

  • MOJA: Kambi ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi.
  • MBILI:
    Simba sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.

    TATU:
    Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.

  • NNE:
    Mo Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.

    TANO:
    Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.

    SITA:
    Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.

    SABA:
    Simba itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika.

    NANE:
    Ameahidi kutenga kitita cha Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja kwa ajili ya usajili.

    TISA:
    Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.

    KUMI:
    Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa