- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: MWINYI HAJJI ATAKA KUONDOKA YANGA KAMA HATA SIKILIZWA
Dar es salaam: Beki wa timu ya taifa ya Zanzibar Haji Mwinyi, anmtaka kocha wa Yanga kumpa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza vinginevyo ataihama club hiyo.
Kiburi hicho cha Mwinyi kinakuja siku chache baada ya kuhitajika na klabu ya FC Leopard ya Kenya, leo mchezaji huyo amekuja na mpya akiitaka klabu yake ya Yanga kumpa nafasi ya kucheza vinginevyo ataomba kuachwa ili akatafute timu ya kuchezea.
Akiongea na muakilishi.com kwa njia ya simu Mwinyi amesema kuwa mbali na FC Leopard kumuhitaji zipo klabu zingine nyingi zinahitaji huduma yake ndiyo maana ametoa angalizo kwa klabu yake ambayo inammiliki impatie nafasi ya kucheza ili kuendeleza kipaji chake na siyo kukaa benchi.
"Natambua kuwa hatuwezi kucheza wachezaji 12, uwanjani lakini kitendo cha kukaa benchi mfululizo kwangu hakinifurahishi kwani nahofia kupoteza kiwango changu nivyema kama sitokuwepo kwenye mipango ya timu basi wanaruhusu kuondoka nikatafute sehemu ambayo nitapewa nafasi ya kucheza," amesema Mwinyi.
Beki huyo ambaye amefanya vizuri kwenye michuano ya Chalenji, akiwa na timu yake ya Zanzibar Heroes waliomaliza nafasi ya pili kwenye michuano iliyomalizika hivi karibuni amesema ataendelea kucheza kwa kujituma ili kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina, kumrudisha kwenye kikosi cha kwanza vinginevyo anapanga kuachana na timu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kwa muda mrefu tangu kuanza kwa msimu huu Mwinyi hajawahi kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kwenye mechi za ligi na kumpisha mgeni Gadiel Michael, aliyesajiliwa kutoka Azam akitamba kwenye nafasi hiyo hiyo mechi zote 11, jambo ambalo limemweka katika wakati mgumu mchezaji huyo.