- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: MODRIC ALIVYOWAPIKU KINA MESSI NA RONALDO
Kiungo wa kati wa kabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia Luka Modric ndio mshindi wa tuzo ya mwaka 2018 ya Ballon d’Or.
Modric, mwenye umri wa miaka 33, hatimaye anakuwa kiumbe wa kwanza kuvunja rekodi ya zaidi ya miaka 10, ambayo imekuwa ikitawaliwa na Cristiano Ronaldo na mchawi Lionel Messi.
Mchezaji huyo, amepata tuzo hiyo, baada ya kuisadia klabu yake kunyakua taji la UEFA Champions League mara tatu mfululizo.
Aidha, alikuwa wa msaada mkubwa, alipoisadia timu yake ya taifa kufika fainali ya kombe la dunia, licha ya kufungwa na Ufaransa mabao 4-2 mwezi Julai huko nchini Urusi.
"Najiskia vema sana. Nimefurahi sana. Nina hisia nyingi sana wakati huu, sina maneno ya kusema,” alisema Modric baada ya kutajwa mshindi, Jumatatu usiku.
Tuzo la Ballon d'Or ilianza kutolewa mwaka 1956, lakini ilianza kushirikiana na FIFA kati ya mwaka 2010 hadi 2015.
Waandaji wa tuzo hii ni Gazeti la Ufaransa la soka la, France Football.
Cristiano Ronaldo ameshinda taji hili mara tano, mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 na 2017 huku Lionel Messi pia akishinda mara tano mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.