- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: MMILIKI WA CHELSEA ABRAMOVICH ACHUKUA URAIA WA ISRAEL
Tajiri wa Urusi anaye miliki klabu ya soka ya Chelsea ya nchini Uingereza Roman Abramovich, amekuwa rasmi Raia wa Israel baada ya nchi hiyo kumpatia haki ya uraia wa nchi hiyo na baadae alisafiri kwa ndege hadi Tel Aviv
Taarifa zinaripoti kuwa alihojiwa na maafisa wa polisi wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Israel mjini Moscow.
Vyombo vya habari vya Israeli vinasema kuwa tayari amepewa kitambulisho cha uraia nchini Israeli chini ya sheria ya kurudi nyumbani, ambayo inawawezesha wayahudi popote pale walipo duniani kurudi na kuwa raia wa Israel.
Gazeti la The Times nchini Israeli limeandika kuwa Bw Abramovich aliwasili Israeli Jumatatu na kwamba amehamia nchini humo.
Uwamuzi wa Bilionea kuyo kwenda Israel ni baada ya kukabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.
Mzozo wa nchi hizo mbili ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal.
Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa.
Viza yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'.
Kucheleweshwa kwa utoaji wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza.
Bwn Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United 1-0.