Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:46 am

SPORT: KOCHA WA SIMBA DJUMA AOMBA MASHABIKI KUMKUBALI

Dar es salaam: Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Masoud Djuma amesema yupo tayari kukabiliana na majukumu aliyopewa na uongozi wa timu ya Simba Sc na kuwataka mashabiki wao kuondoa presha juu yake na kumuamini.

Akiogea na Muakilishi.com kwa njia ya simu Djuma amesema kuwa anauzoefu mkubwa na kazi ya ukocha na ndiyo maana kabla ya kutua Simba, alikwa akiifundisha timu kubwa ya Rayon Sports, ambao ndiyo mabingwa watetezi wa ligi ya Rwanda hivyo haoni kitu kipya ambacho kinaweza kumshinda katika majukumu yake mapya.

"Nakubali kuwa Simba ni klabu kubwa Tanzania, lakini hata mimi nikocha mkubwa ndiyo maana nimeletwa hapa lakini mashabiki wajue kwamba ninauwezo wa kuyamudu majukumu ambayo uongozi umenipa na naamini nitafanya vizuri kwasababu Simba inakikosi kizuri ambacho kinahitaji marekebisho kidogo ili kufanya vizuri," amesema Djuma.

Kocha huyo amesema marekebisha ambayo amepanga kuanza nayo ni katika safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa na makosa mengi kwa kushindwa kufunga mabao kutokana na wingi wa nafasi wanazozitengeneza na baada ya hapo atahamia kwenye safu ya ulinzi lengo ni kuhakikisha hawaruhusu mabao kwenye nyavu zao lakini pia wanafunga idadi kubwa ya mabao kadri wanavyopata nafasi.

Aidha kocha huyo amewaahidi ushindi mashabiki wa Simba, katika mchezo wa ligi ambao unatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii, kwenye uwanja wa Nangwanda Sijana mkoani Mtwara.

"Tayari tumeingia kambini kujiandaa na mchezo huo ambao tumeupa umuhimu mkubwa naamini utakuwa mchezo wa presha kwetu lakini nimewaanda vizuri wachezaji wangu kuhakikisha tunashinda na kurudisha imani ya mashabiki wetu," amesema Djuma.