Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:40 pm

SPORT: KOCHA WA SIMBA ASEMA KIKOSI CHAKE KINAUWEZO WA KUBEBA UBINGWA AFRIKA

Kocha mkuu wa club ya wekundu wa Msimbazi Simba Sport club, amesema ana imani kubwa kuwa kikosi chake kina uwezo wa kupambana na kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

“Kundi lipo wazi kwa timu yeyote kusonga mbele, kwa upande wetu naamini tuna kikosi kinachoweza kushindana na mpinzani yeyote na kupata ushindi.

“Jambo la msingi ni kuunganisha nguvu kwa pamoja kuanzia benchi la ufundi, uongozi na mashabiki ili kuhakikisha azma yetu inafikiwa,” alisema Aussems

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), juzi lilichezesha droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Simba ilipangwa kundi D pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vital ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) na JS Saoura ya Algeria.

Wekundu hao watazindua kampeni zao za hatua hiyo nyumbani Januari 11 kwa kuumana na J.S. Saoura kabla ya kuifuata AS Vita Januari 18 mjini Kinshasa na Al Ahly Februari 1 jijini Cairo kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza.

Simba imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 13, mara ya mwisho ilifanya hivyo mwaka 2003 ilipoitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 3-2, baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani.

Mara hii Simba imefuzu kwa kuitoa Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3, ikichapwa mabao 2-1 ugenini mjini Kitwe kabla ya kushinda mabao 3-1 nyumbani.