- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: KESHO NI FAINALI YA LIGI YA MABIGWA BARANI ULAYA
DAR ES SALAAM: Fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya, baina ya klabu ya Real Madrid na Liverpool itachezwa Jumamosi wiki hii katika Uwanja wa Olimpiki Mjini Kiev nchini Ukraine.
Real Madrid inawania taji la tatu mfululizo la michuano hiyo wakati Liverpool inacheza fainali ya kwanza katika kipindi cha miaka 11.
Mara ya mwsiho Liverpool ilishinda taji hilo mwaka 2005 ilipoifunga AC Milan ya Italia kwa penati 3-2 baada ya timu hizo kufungana mabao 3-3 katika muda wa dakika 120.
Madrid wameshinda taji hilo mara 12, mara ya mwsiho walishinda taji hilo mwaka jana walipoifunga Juventus ya Italia kwa mabao 4-1. Liverpool imeshinda taji la Ulaya mara tano.
Liverpool imefunga jumla ya magoli 46 katika kampeni yao ya mashindano ya Ulaya msimu huu, wakati Reala Madrid ikitegemea zaidi huduma ya mshambuliaji wake Christiano
Ronaldo ambaye katika mchezo wa fainali dhidi ya Juventus alifunga mabao matatu kati ya manne yaliyofungwa na timu yake.
Fainali ya mwaka huu itakuwa ya 63 ya michuano ya Ulaya inayoandaliwa na shirikisho la kandanda barani humo, UEFA.