Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:44 pm

SPORT: JE ? YANGA ITALIRUDISHA TAJI LAKE KOMBE LA FA

Dar es salaam: Mshambuliaji Amiisi Tambwe pamona na kiungo Pius Buswita, wameingarisha klabu ya Yanga Jana baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Reha FC, na kuivusha timu hiyo hadi hatua ya 32, bora ya michuano ya Kombe la FA inayoendelea hivi sasa.

Mabao hayo yamefungwa katika dakika za mwishoni mwa mchezo na kuibua furaha kwa mashabiki wa timu hiyo ambao muda mrefu walikuwa wamekaa kimya wakihofia kuwakuta kile kilichowatokea wapinzani wao Simba juzi.

Hadi dakika 45, za kipindi cha kwanza hakuna timu ambayo ilikuwa imepata bao na Reha licha ya kucheza ligi daraja la kwanza lakini walionyesha kuwasumbua Yanga ambao asilimia kubwa ilitumia wachezaji wa akiba na wale wa timu ya vijana.

Baada ya mapumziko kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa alifanya mabadiliko kwa akimpumzisha Emmanuel Martin na kumuingiza kinda Said Mussa ‘Ronaldo’ aliyekuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Kuingia kwa Ronaldo kuliiongezea kasi ya mashambulizi Yanga na kusaidia kupatikana kwa bao la kwanza dakika ya 82 mfungaji akiwa Buswita aliyepokea paz=si nzuri ya kiungo Papy Kabamba Tshishimbi.

Bao hilo liliwachanganya Raha na kuwapa nguvu Yanga ambapo iliwachukua dakika mbili kuandika bao la pili kupitia kwa mkongwe Amissi Tambwe aliyemlamba chenga kipa wa Reha na kugunga kirahisi na hilo kuwa bao lake la kwanza katika mechi ya pili tangu arejee kwenye kikosi cha Yanga akitokea kwenye majeruhi.

Ushindi huo unaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto zake za kulirudisha taji hilo ambalo lilikuwa linashikiliwa na Simba, ambao tayari wameshaaga michuano hiyo kwa kufungwa na Green Worriors siku mbili zilizopita.