- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: HATIMAYE WAINGEREZA WAANZAA KUTUMIA VAR KWENYE MECHI 60 KUANZIA KESHO
London: ligi kuu ya nchini Uwingereza imeona ni busara kuiga mfumo wa maamuzi unaofanywa na wahispania kwa sasa wa Teknolojia ya kutumia video kuwasaidia waamuzi, maarufu kama Video assistance referee (VAR), teknelogia hiyo inakusudiwa kufanyiwa majaribio katika mechi 60 kwa pamoja katika Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza Jumamosi ya kesho.
Baada ya kujaribiwa katika mechi moja moja msimu uliopita, wasimamizi wa Ligi ya Premia sasa wanataka kuona iwapo teknolojia hiyo inaweza kufanikiwa ikitumiwa katika mechi kadha kwa wakati mmoja.
Majaribio hayo yatakuwa yanadhibitiwa kutoka kituo kimoja kikuu cha VAR.
Hakutakuwa na mawasiliano ya aina yoyote na waamuzi uwanjani mechi zitakapokuwa zikiendelea.
Mechi ambazo VAR itafanyiwa majaribio jumamosi hii
- AFC Bournemouth v Leicester City
- Chelsea v Cardiff City
- Huddersfield Town v Crystal Palace
- Manchester City v Fulham
- Newcastle United v Arsenal
Teknolojia hiyo ya VAR itatumiwa katika uamuzi wa kuthibitisha magoli yanapofungwa, kuamua mikwaju ya penalti, kadi nyekundu za moja kwa moja na kuwatambua wachezaji wakati wa kutoa adhabu, hasa wanapokuwa wengi kwa pamoja kiasi cha kumkanganya mwamuzi.