- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: CLUB YA SIMBA YATUPA KARATA YAKE NYINGINE USIKU WA LEO
Dar es salaam: Leo club ya Simba Sc wanaanza kutetea taji la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kukipiga na Green Warriors, timu zote kutoka jiji la Dar es Salaam, mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia Saa 1:00 usiku wa leo.
Licha ya michuano hiyo kuanza miezi miwili iliyopita, lakini mchezo huo ndio utakuwa maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu huu, kwa sababu Simba ndiyo wanaoshikilia taji baada ya kuwafunga Mbao FC 2-1 katika fainali Mei mwaka huu mjini Dodoma.
Mechi nyingine za leo, Polisi ya Dar es Salaam itamenyana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar es Salaam, iliyohamishia maskani yake Shinyanga; Biashara ya Mara na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani na Madini FC ya Arusha, Mufindi United na Pamba ya Mwanza na Singida United itacheza na Boda Boda FC.
Michuano hiyo itaendelea Jumamosi na Azam FC watacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
Jumapili, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC watacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa; Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.