- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPOETS NEWS : RAMADHANI KISATU AWAZA KWENDA NJE,HATAKI SIMBA WALA YANGA
Kiungo wa timu ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza Athumani Ramadhani Kisatu,amesema kwasasa anafikiria kufika mbali zaidi kisoka kwani hata marehemu mama yake alikuwa akimhusia kujituma katika soka
Ramadhani Kisatu mwenye umri wa miaka 25,ambaye mama yake mzazi alifariki wiki moja iliyopita,ni miongoni mwa wachezaji wakuaminiwa wanaounda kikosi cha mwalimu Thomas zulu katika timu hiyo ya jeshi
Pamoja na ndoto za kucheza soka nje ya nchi kisatu amesema wapo wachezaji wanaocheza soka nje lakini hawajapitia timu za simba na yanga hivyo hajawahi kufikiria kuchezea timu hizo,huku akimtolea mfano mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu
Kiungo huyo wa zamani wa timu ya kanembwe Jkt amefunguka zaidi na kusema sheria hazimruhusu kucheza timu za uraiani,hivyo kwasasa ndoto zake ni kucheza soka nje ya nchi ili kuisaidia nchi na jeshi lake kwa ujumla
"lengo langu nifike mbali zaidi na kufika huko sio lazima nipite yanga au simba,nia yangu ni kuisaidia nchi yangu pamoja na jeshi"alisema Ramadhani Kisatu
Kisatu ambaye amekuwa tegemeo katika upande wa viungo kwenye kikosi cha mwalimu zulu,amekuwa ni mchezaji ambaye mara zote kiwango chake kinapanda kutokana na umahili wake unapokuwa uwanjani