- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SNURA AMVAA FAIZA ALI BAADA YA KUONESHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI
Dar es salaam: Muimbaji na Muigizaji mashuhuri Snura Mushi A.K.A Mama wa Majanga leo juma pili ameshindwa kuvumilia vitendo vya muigizaji mwezake Faiza Ally kuonyesha sehemu za siri za mwili wake kwenye mitandao ya kijamii, picha hiyo zinaonesha Faiza akijufungua akiwa kitandani huku akiwa hana nguo hata moja kwenye sehemu zake za siri za mwili wake. akiandika kwenye Ukurasa wake wa Instagram Snura amesema kuwa leba ni sehem ya siri sana kwa kina mama, yapo mambo ambayo yanafanyika kule hapaswi mwingine kujua wala kuyaona," Faiza ndugu yangu hii umepitiliza TUSITIRI WANAWAKE WENZIO" alisema Snura
"Mwanamke anapotaka kujifungua hata kwa ghafla barabarani zinatafutwa nguo kuziba.... Leba ni siri yetu kina mama kuna mengi tunafanya kule hayastahili kutoka nje niwengi wanashoot mpaka video ila zinabaki kua kumbukumbu zao na sio kuweka hadharani kila mtu akaona inakuaga vipi.'
Snura amesema kuwa kitendo alichofanya Faiza niabu kubwa kwa wanawake na pia kinadhalilisha wanawake wengine " hii niaibu yetu sote tunadhalilika na kupoteza heshima ya mama ..... na tutadharauliwa sana kwa mtindo huu... Hata ndugu zetu wakija hua hawaruhusiwi kuingia leba ni manesi na madaktari tu na kama private basi ataruhusiwa mumeo hizi ndio tamaduni zetu tusijikatae sana na kuutaka uzungu mengine tuwaachie wenyewe sisi tutabaki kua sisi '' alimalizia Snura
lakini posti hiyo ilidumu saa kadhaa kabla ya kufutwa, baada ya kufutwa kwa picha hiyo Faiza alikasirika nakuposti ujumbe huu ''Nimechukia sana picha yangu kufutwa Kwa kweli yaani kweli kuna vitu vya ajabu sana duniani... huku instagram kuna page za wasenge wanafanya mambo ya ajabu, kuna watu wanakata viuno kutwa kuhamasisha ngono, kuna page za wauza papa,kuna page za wauza mikorogo yaani kiufupi kuna page mbaya sana za kuhatarisha jamiii mna acha kuripoti zooote mnaripoti picha yangu ya kuzaa ifutwe kweli ? tatizo liko wapi ? Dah hii kweli ndio bongo vitu vikubwa mnachukulia poa vitu vidogo mnaona big deal how ? Just like how u see mi wa ajabu na mm nakushangaa wewe"
Faiza amekuwa na utamaduni wa kipee wa kutojali sehemu zake za mwili kwa kuposti kwenye mitandao ya kijamii picha zake za utupu, amewahi kufanya hivyo kabla ya kujifugua ambapo alipiga picha zaidi ya 10 na kuziposti mtandaoni huku zikimuonesha muigizaji huyo akiwa kama alivyo zaliwa(uchi).
Faiza ni mzazi mwezie na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi alimaarufu kama SUNGU na walifanikiwa kupata mtoto mmoja aitwae Sasha anaiyesoma shule ya msingi kwa sasa.