Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:34 pm

SEREKALI: NIMARUFUKU MWALIMU KUMPIGA MWANAFUNZI VIBOKO

Dodoma: Serekali ya Tanzania imepiga marufuku mwalimu kumchapa mwanafunzi viboko na pia imepiga marufuku mwalimu kutembea na kiboko akiwa eneo la shule.

Kauli hiyo imetolewa jana Novemba 13, 2018 Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu,(CCM) Rose Tweve.

Bi Rose alitaka kupata ufafanuzi na pia akaitaka Serikali itoe tamko kuhusu walimu kutofuata sheria ya uchapaji wa viboko kwa wanafunzi.

Bi Rose anasema kuna baadhi ya walimu wachache hawafuati taratibu za uchapaji, "naiomba Serikali itoe tamko rasmi kwa walimu wote nchini juu ya wao kufuata sheria za utoaji adhabu kwa wanafunzi,” aliuliza Tweve.

Nae kwa upande wake Naibu Waziri Nasha alisema utaratibu wa viboko umeainishwa vizuri katika Waraka wa Elimu namba 24 wa mwaka 2002, uliotengenezwa chini ya kifungu cha 66 cha sheria ya elimu.

“Mwongozo huo pamoja na mambo mengine umeeleza dhahiri kwamba kuna makosa ambayo viboko vitatakiwa vitumike na siyo kwa kila kosa, bali kwa makosa makubwa ya kinidhamu na yenye sura ya kijinai,” alisema Ole Nasha.
Kuhusu viboko, alisema waraka huo unaeleza wazi kwa wakati mmoja mwanafunzi hatakiwi kuchapwa viboko vinavyozidi vinne.

“Lakini pia anayeruhusiwa kuchapa siyo mwalimu yeyote, bali ni mkuu wa shule au makamu wake au mwingine yeyote aliyepewa ruhusa hiyo kwa maandishi.

“Kitu kingine kinachoelezwa katika waraka huo ni kuchapa viboko lazima kibali, na kitolewe na mkuu wa shule kwa maandishi maana waraka unasema waziwazi kwamba ni marafuku mwalimu yeyote kutembea na kiboko kwa ajili ya kumchapa mwanafunzi,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwaagiza maofisa elimu wote kuhakikisha wanagawa waraka huo kwa walimu ili wausome na wautekeleze.

Akijibu, Ole Nasha alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua kwa wanaobainika kujihusisha na vitendo vya kikatili au unyanyasaji dhidi ya watoto kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi na sheria za nchi.

“Mfano walimu waliohusika kumpiga mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta iliyopo Manispaa ya Bukoba na kusababisha kifo chake walisimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani na kesi inaendelea, na ofisa elimu kata, mwalimu mkuu na msadizi wake wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi,” alisema.