Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:43 am

SAKATA LA LULU LAWAGOMBANISHA AFANDE SELE NA MRISHO MPOTO

Dar es salaam: Wakali wawili wa mashairi wa muziki wa Bongo fleva Tanzania Selemani Msindi A.K.A Afande Sele na Mrisho Mpoto alimaarufu kama Mjombo wameingia kwenye vita ya maneno baada ya Mresho Mboto kujibu post aliyoiposti mkali wa mashari Afande sele kwenye ukurasa wake wa Instagram Juu ya Utata wa kifo cha muigizaji Steven Kanumba na Uhusiano kati ya Kanumba na Lulu.

Afande sele alikasirishwa na kitendo cha muigizaji Steven kanumba kutoka na Lulu kwa kipindi kile, akiamini kuwa Lulu alikuwa binti mdogo ambaye alitakiwa kusoma na kufanikisha malengo yake, na hiyo ndio ikawa sababu ya Afande kutoshiriki msiba wa Kanumba "lkn niliumia zaid baada ya matatizo aliyoyapata lulu kupitia kanumba na kwa hakika sikua miongoni mwa waliohuzunika wala kushiriki kivyovyote ule msiba wa kanumba ingawa wkt wote wa pilika za msiba ule mimi nilikua dar tena palepale sinza msiba ulipokuwepo...sikutaka kuvaa joho la unafki kama ilivyo kwa waTz wengi...kwangu hata sasa kanumba ni mtu mbaya na alifanya kitendo kibaya kabisa dhidi ya bint mdogo aliyepaswa kumsaidia kufikia malengo na sio.kumtumia kwa sababu ya umaarufu wake" alisema AFANDE

Naye Mrisho mpoto baada ya kauli hiyo ameonesha kutoridhika na maneno hayo ya mfalme wa Mashari na kutaka ufafanuzi juu ya chiki yake hiyo kwa msanii kanumba

"Kaka yangu Afande Sele.. Mfalme wa maandishi...!! afandeseleking Wewe ni Kaka yangu na ni mwandishi ambae sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako ...Leo nna mambo kadhaa kidogo kwako Kaka yangu.... Nimesoma maandishi kwenye ukurasa wako zaidi ya mara 30 Huku nikiyarudia rudia mara Kadhaa...ningependa kujua vitu Vichache kabla ya hoja yangu ya msingi kuiweka mezani...ile Barua ulimwandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie? Au ulitaka wanaokwenda nyuma yake wamfikishie?


"ulitaka waliopo wajifunze kupitia walaka wako? Mbona nimepata kusikia Marehemu huwa halaumiwi kwakua hana uwezo wa kijitetea? Umesema ulikuwepo Sinza wakati wa msiba na hukutaka kusogea wala kuzika kwakua unasema wewe siyo mnafiki kama watanzania waliokwenda kuzika... ikiwa watu wote wangekataa ile Maiti ingekuaje? Nini Hasa lengo la Movies za Kibonge kuziita Maigizo yanayowekwa Kwenye Kanda? una ugomvi na Bongo Movies au uliandika ukiwa kwenye Jazbda kidogo....!! Mimi ndugu Mrisho Mpoto"